Misingi imara ya ukaguzi yaipaisha NBAA Afrika

DAR ES SALAAM: Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) imeeleza kuwa moja ya sababu zilizochangia Shirikisho la Wahasibu Barani Afrika (PAFA) kuichagua Tanzania kuwa kituo cha umahiri wa uandaaji wa ripoti za fedha zinazozingatia mazingira, jamii na utawala bora ni kutokana na kuwa na misingi imara ya uhasibu na ukaguzi barani humo.
Akizungumza katika warsha ya siku nne ya uwasilishaji wa taarifa endelevu za kihasibu, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno amesema mafunzo hayo yatasaidia kuhamasisha wahasibu kushiriki katika kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
SOMA ZAIDI
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dk. Germana Leya amesema mafunzo hayo yatachochea uendelevu na usalama wa mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Aidha, Mkuu wa Rasilimali Watu na Utawala wa NBAA, Gloria Kaaya, amesema warsha hiyo inalenga kuhakikisha taasisi na wataalamu wa uhasibu wanajengewa uwezo wa kuandaa taarifa zinazozingatia utawala bora na maendeleo endelevu.
Warsha hiyo ya siku nne imewashirikisha takribani wahasibu, wakuu wa taasisi na maafisa rasilimali watu 500 kutoka taasisi mbalimbali nchin