Mjumbe INEC ataka uadilifu uchaguzi mkuu

MOROGORO: WASIMAMIZI na wasaidizi wa vituo vya kupigia kura wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki, amani na uwazi.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Asina Omari, ametoa wito huo alipozugumza na wasimamizi hao kwenye mafunzo katika Kituo cha Tarafa ya Mvomero, ambayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Sokoine Memorial, wilayani Mvomero.
Mafunzo hayo yaliyoanza Oktoba 26 hari 27, mwaka huu katika vituo vya tarafa ya Mvomero, Mlali na Turiani wilayani humo.
Jaji Asina amesema INEC imeweka utaratibu na miongozo kuhakikisha kila hatua ya mchakato wa uchaguzi inazingatia sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi, hivyo ni wajibu wa kila msimamizi kuhakikisha anasimamia kwa weledi bila upendeleo.
Hiivyo amewataka kuhakikisha kuwa wanazingatia suala la muda wa kufungua vituo na kufunga vituo vya kupiga kura akisisitiza kuwa kuwahi kwao kutaondoa malalamiko.
Mbali na hayo ,Jaji Asina amepata fursa ya kukagua baadhi ya vituo wazi vya kupigia kura katika kata ya Dakawa kikiwemo kituo cha Ofisi ya Serikali ya kijiji cha Dakawa.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mvomero, Mary Kayowa akiwa katika kituo cha Tarafa ya Mlali kuangalia utoaji wa mafunzo kwa wasimamizi hayo amewakumbusha wote kutunza siri , nidhamu, uadilifu na weledi katika utendaji wao kwani ni nguzo kuu za kuhakikisha uchaguzi wa amani na wa haki.

Amewataka kutekeleza majukumu yao kwa kufuata maelekezo yote ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Kayowa amewataka wakahikishe wanawapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu, wanawake wajawazito, wenye watoto wachanga na wazee .
Amesema kwa wale wenzetu ambao hawaoni kutakuwa na matumizi ya nukta nundu kwa ambao wanaweza kuzitumia kutakuwa na karatasi hizo na wataweza kutumia ili kupiga kura vizuri ikiwemo na matumizi vitotori ambavyo ni rafiki kwa watu wote kwa ambao sio walemavu na wenye ulemavu.
Naye ,Msimamizi wa Kituo, Jamila Seif ambaye ni miongoni mwa walipatiwa mafunzo hayo amesema watakwenda kusimamia uchaguzi huo na kwamba utakuwa huru na haki kwa watanzania wote kutokana na kujengewa uwezo na uwelewa wakutosha katika kuwezesha kuifanya kazi hiyo kwa mujibu wa sheria , kanuni na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba 29, 2025 ambao umebeba kauli mbinu “Kura yako Haki yako, Jitokeze Kupiga Kura” ambapo watanzania watajitokeza kuchagua viongozi wao watakao waletea maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com