Mjumbe Kamati Kuu CCM atoa somo upigaji kura

ARUSHA: MJUMBE wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Namelok Sokoine ametoa somo la elimu ya jinsi ya kupiga kura kwa jamii ya kifugaji ya Kimasai katika Kata ya Engaranaibor Wilayani Longido Mkoani Arusha ili kura za jamii hiyo zisiweze kuharibika.
Namelok alisema ana amini kuwa kila mmoja ana kadi ya kupigia kura na kadi hiyo inapaswa kutumiwa vizuri na wananchi wa jimbo hilo ambao wengi wao ni wafugaji wa Kimasai namna ya kupiga kura kwa mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Mbunge na Madiwani ili waweze kumsaidia Rais kusukumu maendeleo ya Jimbo la Longido.
Alisema yeye hana maneno mengi kwa siku ya leo kwa kuwa mgeni rasmi katika ufungaji kampeni na kusema eneo la Engaranaibor lina histori kubwa sana katika familia ya Sokoine hivyo alipoombwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Longido, Dk Steven Kiruswa hakusita na alikubali mwaliko huo.
Mjumbe wa huyo wa Kamati Kuu ya CCM aliwataka wakazi wa Longido kuhakikisha wanashika nafasi ya kwanza kimkoa na ikiwezekana Kitaifa kwa kura za ndio kwa mgombea Urais wa CCM Samia Suluhu Hassan ili aweze kuendeleza yale aliyoyafanya na anayotaka kuyafanya kwa maslahi ya wananchi wa Jimbo la Longido.

“Amewataka wanawake wa jinsi zote wadogo lwa wakubwa,vijana na wazee kujitokeza kwa wingi kesho kwenye vituo vya kupiga kura lengo ni kumchagua Rais Samia awe Rais kwa awamu nyingine tena ya kuliongoza Taifa”alisema Namelok
Kabla ya hotuba za viongozi mbalimbali wa CCM,Namelok alifanyiwa maombi maalumu na viongozi wa dini zote na viongozi wa Milla wa Kimasai maarufu kwa jina la Malaigwanani ili aweze kuendelee vema kuongoza chama mkoa na taifa pia kumwombea Rais afya njema ili aweze kuongoza vema Taifa la Tanzania.
Mwwnyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy ole Sabaya amesema kuwa jimbo la Longido hususani kata ya Engaranaibor ina histori kubwa kwa familia ya Sokoine hivyo basi wananchi wa Tarafa ya Engaranaibor wanapaswa kuienzi historia hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa kura nyingi kwa Rais ili kuwaheshimisha wana Longido kwa ujumla.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido, Dk Steven Kiruswa ambaye alihutubia mamia ya wakazi wa kata ya Engaranaibor kwa mvua kubwa alisema wananchi wa jimbo hilo hawamdai mgombea Urais wa CCM,Samia Suluhu Hassan kwani amefanya mambo malubwa ikiwemo kupeleeka miradi ya maendeleo ya zaidi ya Sh bilioni 106.

Kiruswa alisema Longido itakuwa ya kwanza kuongoza katika kura ya Rais kwani wananchi wa jimbo hilo wanamkubali sana kwa kuwa amewajali kwa miradi ya maji,elimu,afya na barabara hivyo fadhila yao ni kumpa kura za kishindo ili aweze kuongoza tena nchi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafayabiashara wa Madini (CHAMMATA), Jeremia Kituyo amesema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa katika sekta ya madini hivyo anapaswa kuchaguliwa tena kuliongoza Taifa ili aweze kukamilisha ama.kuboresha zaidi sekta hiyo ambayo ni muhimili mkubwa wa nchi.

Kituyo alisema sekta ya madini ilikuwa chini katika kuliingizia Taifa Mapato lakini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na usimamizi mzuri wa mawaziri na watendaji wa Wizara hiyo sasa sekta hiyo imekuwa tegemeo la Taifa katika kuingoza mapato na imekuwa ikivuka malengo ya ukusanyaji mwaka hadi mwaka.




Begin now earning every month an extra amount of $17k or more just by doing very simple and easy online job from home. I have received $18953 in my last month direct in my bank acc by doing this easy home base job just in my part time for 2 hrs maximum a day online. Even a child can now do this job and earns money online. Everybody can get this home job right now and start earning dollars online by follow details here……….
Click the link—↠ https://www.Homeprofit1.site
I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:
COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site
I am making effectively tirelessly $15k to $20k basically by doing coordinate work at domestic. Multi month once more i have made $45890 from this development. astounding and smooth mac to do work and standard pay from this can be stupefying. i have propose each last one of you to connect this advance right specifically as moo security and get than full time compensation through take after this affiliation.
:
) AND Great Good fortune.:
)
HERE====)> https://cashprofit7.site