Mkongo wa mawasiliano kujengwa Sikonge-Inyonga

DODOMA; SERIKALI imesema imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kuwa ni muhimili wa mawasiliano hapa nchini.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hayo bungeni leo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Restituta Mbogo aliyehoji ni lini serikali itajenga Mkongo wa Mawasiliano katika eneo la Sikonge hadi Inyonga mkoani Tabora.

“Katika mwaka huu wa fedha 2023/24 Serikali imepanga kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuanzia Tabora-Sikonge-Inyonga Majimoto-Kizi wenye urefu wa Kilomita 369. –

“Hadi sasa serikali kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imesaini mkataba na Mkandarasi kwa ajili ya kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika maeneo hayo.

“Hatua za utekelezaji zimeanza ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2024,”amesema Waziri Nape.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button