Mloganzila yaandaa kambi kupandikiza nyonga, magoti

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila imeandaa kambi maalumu ya upasuaji wa marejeo wa kupandik iza nyonga na magoti kuanzia Februari 26 hadi Machi 7, 2025.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili Mloganzila, Dk Godlove Mfuko alisema wamean daa kambi hiyo kwa kushirikiana na daktari bingwa mbobezi wa upasuaji na upandikizaji wa nyonga, magoti na viungo vingine bandia kutoka Hospi tali ya Chuo kikuu cha Peking Third ya China, Profesa Tian Hua.
Dk Mfuko alisema Profesa Hua atakuja maalumu kwa ajili ya kuwa jengea uwezo madaktari wa Tanzania ili wakati mwingine changamoto hizo zisiwe sababu ya wagonjwa kupewa rufaa kwenda kutibiwa nje ya nchi kwani gharama huwa kubwa.
Aidha, Dk Mfuko alisema upasuaji huo ulikuwa haufanyiki nchini kwa kuwa kulikuwa hakuna vifaa hivyo bandia na pia kukosekana kwa wata alamu.
“Mara hii itatujengea uwezo kwa wataalamu wetu ili tuweze kuwa tunazifanyia hizi operesheni kama kawaida, hakuna haja ya mtu kupewa rufaa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya operesheni hizi,” alisema.
Alisema kwa kawaida upasuaji wa marudio wa kubadilisha nyonga na magoti hufanyika baada ya kipindi cha miaka 10 hadi 15 baada ya upa suaji wa mwanzo, kwa kuwa viungo bandia hivyo hulika na kusababisha maumivu kwa mgonjwa.
“Operesheni za mwanzo ambazo tumeanza kuzifanya kama ambavyo tumekuwa tukiwatangazia, sasa hivi tumeshafanya zaidi ya operesheni 252 kwa kipindi cha chini ya miaka miwili iliyopita, za magoti tumefanya kama 192 na zilizobaki tumefanya za nyonga kwa ufanisi na mafanikio makubwa sana,” alisema.
Dk Mfuko alitoa wito kwa ambao wamewahi kufanyiwa upasuaji wa magoti au nyonga waende hospitalini hapo mapema ili waweze kufanyiwa vipimo na uchunguzi mapema.



