Mobetto kupamba Tanzania Fashion Festival

MWANAMITINDO na msanii maarufu wa Bongo Movie, Hamisa Mobetto, anatarajiwa kupamba usiku wa Tanzania Fashion Festival utakaofanyika Oktoba 18 katika ukumbi wa Delta Hotel, Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na HabariLeo, Msemaji wa Tamasha Hilo , Bhoke Egina, amesema mwaka huu wameamua kuvunja mtindo wa zamani kwa kuwaleta wanamitindo wenye maumbo halisi ya Kiafrika. “Kwa muda mrefu tasnia ya mitindo imekuwa ikihusishwa zaidi na wasichana warefu wembamba. Safari hii tumeamua kuonesha kuwa hata wanawake na wanaume wenye maumbo ya Kibantu wanaweza kuonekana vizuri katika mavazi ya kisasa,” amesema Bhoke .
Amefafanua kuwa jina la Hamisa Mobetto liliibuka kwa ajili ya kufungua tamasha hilo kutokana na muonekano wake wa Kiafrika, umaarufu na mchango mkubwa alioutoa kwenye tasnia ya mitindo. “Hamisa ana mvuto wa kipekee, umbo la Kibantu na huvaa mavazi ya mitindo kwa ufanisi mkubwa. Kwa sasa tunaweza kusema ameliteka soko la mitindo Tanzania,” ameongeza.
Kithama amesema lengo kuu la tamasha hilo ni kutoa nafasi kwa wabunifu chipukizi pamoja na nguli wa mitindo kuonesha vipaji vyao, huku wakipinga dhana potofu kwamba mitindo ni ya watu wembamba pekee. Mbali na Hamisa, wasanii wengine waliotajwa kushiriki ni pamoja na Jux, Phina na Nandy, ambao nao wamekuwa mstari wa mbele kuendeleza tasnia ya mitindo nchini.
Aidha, Bhoke ametoa wito kwa kampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini tamasha hilo, amesisitiza kuwa washiriki wa mitindo hawatalipia gharama yoyote, huku mapato ya viingilio yakitumika kugharamia maandalizi. Viingilio vitakuwa kama ni Sh20,000 (kawaida), Sh60,000 (VIP) na Sh1,000,000 kwa meza ya watu 10 (VVIP). SOMA: Jubilant Andrew: Mitindo ipewe thamani inayostahili
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com