Zaidi ya 40 wapoteza maisha Hong Kong

ZAIDI ya watu 40 wamethibitishwa kufariki dunia katika moto mkubwa ulioteketeza majengo kadhaa ya ghorofa jijini Hong Kong. Watu wengine 45 wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya, huku zaidi ya 279 wakiripotiwa kutopatikana hadi sasa.

Polisi wamewakamata watu watatu kwa tuhuma za mauaji, wakiwemo wakurugenzi wawili wa kampuni ya ujenzi na mshauri mmoja wa masuala ya uhandisi. Wakati uchunguzi wa chanzo cha moto huo ukiendelea, polisi wamegundua wavu na makaratasi ya plastiki yalipatikana yakifunika madirisha ya majengo wakati wa ukarabati  huenda ikawa chanzo cha moto huo kuenea kwa kasi .

Mapema leo Novemba 27, moshi ulikuwa bado unafuka kutoka baadhi ya majengo, ingawa moto umedhibitiwa katika majengo manne kati ya manane.Idara ya Zimamoto ya Hong Kong imesema inaweza kuchukua siku nzima kuuzima  moto huo kikamilifu.

Mamia ya wakazi wamehamishwa na kupelekwa kwenye makazi ya muda pamoja na nyumba za dharura zilizotengwa kwa walioathrika na moto huo. Kwa mujibu wa Idara ya Zimamoto, huu ni moto mkubwa zaidi kuwahi kutokea Hong Kong katika kipindi cha miaka 17. SOMA: Jamii yaagizwa kuchukua tahadhari ya moto

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button