Wanasayansi wazindua dawa kulinda vifaru

AFRIKA KUSINI : WANASAYANSI nchini Afrika Kusini wamezindua mradi wa kisayansi wa kutumia dawa zenye mionzi kudunga pembe za kifaru kama njia ya kupambana na wawindaji haramu.

Kwa mujibu wa watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand, mionzi hiyo haitakuwa na madhara kwa afya ya wanyama, bali itasaidia kuimarisha juhudi za udhibiti wa usafirishaji haramu wa pembe kwenye viwanja vya ndege na bandari.

Mradi huo ujulikanao kama Rhisotope, umezinduliwa rasmi baada ya miaka sita ya utafiti na majaribio, na unatarajiwa kuleta mapinduzi katika vita dhidi ya uwindaji haramu wa wanyamapori barani Afrika. SOMA:Mamlaka Ngorongoro yadhibiti ujangili

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button