MRADI wa Bomba la Mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP) unaotoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga Tanzania umefikia asilimia 45.5 na tayari Sh bilioni 977 zimetolewa na serikali ya awamu ya sita katika utekelezaji wa mradi huo.
Hayo yamesemwa leo na mratibu wa mradi huot aifa kutoka Shirika la Maendeleo la Petroli nchini (TPDC) Asiadi Mrutu wakati wa ziara ya kukagua Maendeleo ya kiwanda cha kuweka mifumo ya kupasha na kutunza joto kilichopo kijiji Cha Sojo kata ya Igusule wilayani Nzega mkoani Tabora.
Mrutu akiwa ameamb atana na kamati ya usimamizi wa madeni ya taifa pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC Taifa walipongeza kwa hatua inavyokwenda kwa Kasi ya mradi huo na utolewaji wa ajira kwa Watanzania 7584 sawa na asilimia 94.
“Mpaka sasa fedha zilizotolewa juu ya utekelezaji wa mradi huu ni Sh bilioni 977 pia Sh bilioni 856 zimelipwa kwa watoa huduma mbalimbali wanaofanya kazi kupitia mradi, “amesema Mrutu.
Naibu katibu Mtendaji wa Tume ya Kitaifa ya Mipango anayesimamia Masuala ya Menejimenti ya Miradi ya Maendeleo Linda Ezeckiel amesesema kiwanda hiki kitasaidia kuyeyusha Mafuta ambayo yatakuwa yameganda kutoka yanapoanzia kimeleta ushirikiano mzuri kwa Taifa na wakazi wanaozunguka eneo hili.
Mambomba 86000 yatawekewa mfumo wa joto na mpaka Sasa mambomba 3000 yamekwisha wekewa mfumo na hapo hali inatuhalalishia ifikapo mwaka 2026 utakuwa umekamilika kwa asilimia 100.
Ezeckiel amesema upande wa Tanzania umewekeza kilomita zaidi ya 1000 Kati ya kilomita 1443 zinazoanzia Hoima nchini Uganda na tayari baadhi ya Watanzania wamepelekwa nchini Ujerumani kupata utaalamu zaidi na wengine wanaoshiriki katika ujenzi huu wanao uwezo wa kuuelezea vizuri zaidi.
Mjumbe wa bodi ya TPDC Balozi Peter Kallaghe amesema wamekuja kuangalia kwani tangu kifunguliwe mwezi Machi mwaka huu na Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko yamefanyika Maendeleo makubwa na matarajio ifikapi mwaka 2026 kitaanza kufanya kazi.