Mradi wa maji miji 28 suluhu Tanga

MRADI wa maji wa miji 28 unaotekelezwa katika wilaya nne za mkoa wa Tanga unakwenda kumaliza kabisa changamoto ya ukosefu wa maji.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema hayo leo Novemba 16 alipotembelea eneo la chanzo cha maji Tabora kilichopo Kijiji cha Mswaa wilaya ya Korogwe mkoani humo.

Advertisement

 

Amesema mradi huo unaotarajiwa kugharimu shilingi bilioni 170 hadi kukamilika kwake utanufaisha wananchi wa wilaya za Muheza, Pangani, Handeni na Korogwe.

SOMA: Maji ya Wami/Ruvu kunufaisha Μkata

“Mpaka sasa mradi umekufikia zaidi ya asilimia 60 hivyo niwaombe wakandarasi kuhakikisha mnakamilisha mradi huu kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika,”amesema Aweso.

Aidha Waziri Aweso amewataka wananchi wa kata ya Mswaha kuwa walinzi wa miundombinu ya mradi huo ambao umegharimu fedha nyingi.

 

Awali wananchi wa eneo hilo wameishukuru serikali kwa mradi huo utakaowaepusha na madhara mbalimbali yakiwemo kuliwa na mamba wanapokwenda kutafuta maji.