Msumbiji yakumbwa ongezeko la wakimbizi

MSUMBIJI : SHIRIKA  la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji (IOM), limeeleza kuwa mashambulizi ya waasi katika mkoa wa Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji, yamesababisha zaidi ya watu 46,000 kuyahama makazi yao katika kipindi cha siku nane mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa IOM, takribani asilimia 60 ya waliokimbia makazi yao ni watoto, ingawa hakukuwa na taarifa rasmi za vifo vilivyotokea kutokana na mashambulizi hayo. SOMA: Wahamiaji haramu 126 wadakwa Geita

Ripoti ya Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa wimbi la mashambulizi hayo lilijitokeza kati ya Julai 20 hadi 28 katika wilaya tatu za Cabo Delgado, na kusababisha ongezeko la watu waliolazimika kuhama.

Umoja wa Mataifa umewatuhumu wanamgambo wa jihadi kwa vitendo vya ukatili ikiwemo kukata vichwa vya wanavijiji na kuwatumikisha watoto kama askari au vibarua. Aidha, Umoja huo umeeleza kuwa vurugu, ukame na vimbunga vilivyolikumba eneo hilo kwa miaka ya hivi karibuni vimesababisha zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao kaskazini mwa Msumbiji.

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button