Mtambo wa kisasa uchimbaji madini wazinduliwa

DAR ES SALAAM;  MTAMBO wa First Franna FR17 C ni miongoni mwa mitambo mikubwa ya kisasa utakaotumika katika shughuli za uchimbaji madini nchini .

Akizungumza katika uzinduzi wa mtambo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk Venance Mwasse, amesema mtambo huo unaweza pia kutumika kwa shughuli zingine zikiwemo ujenzi wa viwanja vya soka.

Amesema mtambo huo uliotengenezwa na Kampuni ya Meta Group Africa wauzaji mashine za uchimbaji madini, utengenezaji wa barabara na utiririshaji ardhi wanaofanya kazi Afrika Mashariki na Kusini umezinduliwa usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mtambo huo wenye uwezo wa kubeba mgizo wa tani 17, urefu ‘boom’ ni meta 18.23 ni wa kwanza Tanzania.

Soma: BOT kuwawezesha mitaji wachimbaji Madini

“Vile vile Shirika la Madini la Taifa ni mlezi wa wachimbaji wadogo, wanahitaji kupata vifaa kama nilivyowaambia wajaribu kutengeneza vifaa vyenye saizi ndogo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, kwa sababu vifaa vikubwa kwa mchimbaji mdogo ni mzigo,” amesema na kuongeza:

‘Kwa hiyo wakiweza kuvipunguza saizi vikawafaa wachimbaji wadogo, tunawahakikishia watapata soko kubwa kwa wachimbaji wadogo na sisi kama Stamico tutahakikisha hilo linafanyika,” amesema Dk Mwasse.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)


Kampuni ya Meta Group Africa inafanya kazi katika nchi za Angola, Rwanda, Tanzania, Kenya na Uganda. Lakini pia inatengeneza vifaa, vichanganyaji, pampu na mitambo ya kubandika kutoka Schwing Stetter na SIRL kwa ajili ya masoko ya Kenya, Tanzania na Rwanda.

Habari Zifananazo

Back to top button