Mtanzania atoa elimu ya usalama majini

AFRIKA YA KUSINI: Mtanzania Moses Ntilema ambaye ni mwezeshaji wa programu ya taifa nchini Afrika Kusini iitwayo WATERSMART ameshiriki vema kutoa elimu ya usalama majini katika kuadhimisha ‘Madiba Day’.
Madiba Day ni siku ya kitaifa ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela ambayo hufanyika kila tarehe 18 Julai.
SOMA: www.https://www.un.org/en/events/mandeladay/mandela_prize.shtml
Ntilema anayeishi Afrika Kusini pia ni mwakilishi ndani ya Wilaya ya Nelson Mandela Bay katika kutoa elimu ya usalama majini kwenye shule zote za serikali na binafsi nchini Afrika Kusini.
Alizungumza na HABARILEO ONLINE kutoka Afrika Kusini jana Ntilema alisema mradi huu umedhaminiwa na DHL na Princess Charlene of Monacco Foundation South Africa.
“Hii ni katika kujiandaa kuadhimisha siku ya Usalama na Kuzuia maafa majini Duniani yaani (World Drowning Prevention Day) ambayo ni tarehe 25 Julai ya kila mwaka.”
SOMA: https://habarileo.co.tz/taasisi-ya-mandela-yaiomba-serikali-mazingira-safi-ufundishaji/Ntilema
alisema anajisikia fahari kutoa mchango wake kwa wanafunzi lakini ndoto yake ni kuona siku moja anawafikia wanafunzi wa Tanzania kwa lengo la kuwapa elimu ya kijikinga na maafa ili kuokoa maisha ya wengi.



