MV Butiama Hapa Kazi yaanza safari Ukerewe

MWANZA: MELI ya MV Butiama Hapa Kazi imeanza safari zake upya leo Septemba 20, 2025 kutoka Mwanza kwenda Wilaya ya Ukerewe, baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa muda wa miezi tisa.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko Kampuni ya Meli Tanzania (Tashico), Anselm Namala, amesema wakati wa sherehe za upokeaji wa meli hiyo wilayani Ukerewe kwamba:

Desemba, 2024, MV Butiama ilipata hitilafu ya mizania, iliyoipelekea kwenda upande, hatimaye kupaswa kupelekwa haraka kwenye karakana Mwanza.

“Tunaomba radhi kwamba matengenzo yamechukua muda mrefu, ni kwa sababu kwa namna yoyote ile tusingeweza kuhatarisha usalama wa abiria, watumishi wa meli, na chombo chenyewe.

“Sasa meli imerudi kazini na iko salama kabisa kwasababu siku tatu kabla ya kuanza safari tulishirikiana na wadau wengine wa usafiri wa kwenye maji, hasa Chuo cha Bahari Dar es Salaam na Shirika la Uwakala wa meli Tanzania kuifanyia majaribio kadhaa.”

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ukerewe, Khamis Mambile, naye amepongeza serikali kuboresha usafiri wa kwenye maji kwani mbali na MV Butiama kurudi kazini, ujenzi wa vivuko viwili umekamilika na vitaanza kazi hivi punde katika visiwa vya Bukondo-Bwiro, na Lugezi Kisorya wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Christopher Ngubiagai, amesema uboreshaji wa usafiri wa kwenye maji una faida nyingi kiuchumi na kijamii, hasa kurahisisha usafiri wa wananchi na mazao kwenda katika masoko jijini Mwanza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button