Mvomero kuboresha soko la Nyandira

MOROGORO : WAKULIMA wa Tarafa ya Mgeta, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wameiomba Serikali pamoja na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kukaa pamoja kutatua changamoto zinazolikabili Soko la Nyandira ili kulifanya liwe endelevu na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi, halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Wakulima hao walitoa ombi hilo wakati walipomshukuru Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Anne Sophie Avé, aliyefanya ziara katika soko hilo ambalo Serikali ya Ufaransa ilifadhili ujenzi wake.
Mkulima wa kikundi cha Bega kwa Bega na Mwanamtandao wa Kata ya Tchenzema, Otensia Thomas, alisema soko hilo lilijengwa na MVIWATA kwa ufadhili wa Serikali ya Ufaransa baada ya wazo hilo kuibuliwa na wakulima mwaka 2002, na mradi wa ujenzi kukamilika mwaka 2004.
Amesema kuwa awali, wakulima wenyewe walikuwa wanasimamia soko hilo kwa makubaliano maalumu kati ya Serikali, Halmashauri na MVIWATA. “Soko hili kimsingi limekuwa msaada mkubwa kwa wakulima wa Tarafa ya Mgeta na Wilaya ya Mvomero. Wameweza kuinua hali zao za maisha, kujenga nyumba bora, kuwasomesha watoto na wengine kujiajiri katika shughuli za ushonaji na mama lishe katika eneo la soko,” alisema Otensia.
Ameongeza kuwa tangu mwaka 2016, soko hilo lipo chini ya usimamizi wa Serikali huku MVIWATA ikiendelea kufuatilia namna vikundi vya wakulima vinavyonufaika nalo. Hata hivyo, alisisitiza kuwa soko linahitaji kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara ili liendelee kuwa na tija.
Naye mkulima na mkazi wa Nyandira, Bononasi Mwiache, alisema ujenzi wa soko hilo pamoja na barabara ya zege umeondoa adha kubwa kwa wakulima waliokuwa wakitembea zaidi ya kilometa 15 kubeba mizigo yao kwenda Soko la Langali. “Kabla ya ujenzi wa soko hili, tulikuwa tunatembea umbali mrefu kubeba mizigo kichwani hadi Langali. Sasa tuna soko letu hapa kijijini na tunauza mazao kwa urahisi,” alisema Mwiache.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero , Maulid Dotto, aliwahakikishia wakulima kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo kwa haraka, ikiwemo kuboresha miundombinu ndani ya soko hilo ili kuwawezesha kuendelea kunufaika na kilimo.
Balozi wa Ufaransa nchini, Anne Sophie Avé, aliwapongeza wakulima hao kwa kutumia vizuri soko hilo na kuwataka waongeze uzalishaji wa mazao yenye ubora yatakayoweza kushindana katika masoko ya kimataifa. “Tanzania na Ufaransa zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika sekta ya kilimo. Mfano wa Soko la Nyandira ni wa mafanikio ya ushirikiano huo kwa zaidi ya miaka 30,” alisema Balozi Avé.
Aliongeza kuwa alifurahishwa kuona wakulima wa Nyandira wakifanya kazi kwa bidii, wakilima katika mashamba ya milimani na kuzalisha mazao ya ubora wa juu. “Nimefurahia pia kuona chakula cha asili cha Kitanzania kikiandaliwa wakati wa chakula cha mchana. Hii ni ishara ya uzalendo na utunzaji wa tamaduni,” alisema. SOMA:a bei za m Samia: Samia: Tutalinda bei za mazao
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com