MTUME Boniface Mwamposa wa Kanisa la Arise and Shine (Inuka Uangaze), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na mmiliki wa Kampuni ya Utalii ya Leopard Tour wametoa pikipiki 60 kwa Jeshi la Polisi Arusha ili kuendeleza jitihada za kuimarisha ulinzi na usalama.
Pikipiki hizo 20 kutoka kwa Mwamposa, 20 kutoka NSSF na 20 kutoka kwa Leopard Tour zimetolewa na kukabidhiwa leo nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, ambapo Boniface Mwamposa ameahidi kuendelea kujitoa kwa wananchi wa Arusha.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Justine Masejo wameshukuru kwa msaada huo, huku RPC Masejo akiahidi kuzitumia kikamilifu pikipiki hizo katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa Mkoa wa Arusha unaimarika.