Mwasongwe awatia moyo mashabiki

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Ambwene Mwasongwe, amewapa mashabiki na Watanzania ujumbe wa faraja na matumaini, akisisitiza umuhimu wa kumtegemea Mungu katika kila hatua ya maisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwasongwe aliandika ujumbe ulioigusa mioyo ya wengi, akieleza kuwa bila msaada wa Mungu hakuna mwanadamu anayeweza kusaidia kwa ukamilifu, lakini mara Mungu anaposaidia hakuna cha kuogopwa wala kinachoweza kushinda.

β€œMungu asipotusaidia hakuna atakayetusaidia. Ila Mungu akitusaidia hakuna wa kututisha wala kutushinda. Nakuombea uzima, afya na amani unapojiandaa kuvuka mwaka huu,” aliandika Ambwene. SOMA: Rose Muhando afunika Mtoko wa Pasaka

Ujumbe huo umepokelewa kwa hisia chanya na mashabiki wengi, ambao wameendelea kumpongeza kwa kutumia jukwaa lake kueneza maneno ya matumaini, imani na upendo, hususan katika kipindi hiki cha mabadiliko ya mwaka.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. β˜…ε½‘[𝐍𝐄𝐄𝐃 ππ„πŽππ‹π„ π…πŽπ‘ 𝐏𝐀𝐑𝐓 π“πˆπŒπ„ πŽππ‹πˆππ„ π–πŽπ‘πŠ]ε½‘β˜…

    Start making cash right now… I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my befst friend earns over $19,000 a month doing this and she convinced me to try. ift was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by visiting Following Link…

    π‡πžπ«πž 𝐒𝐬 𝐈 𝐬𝐭𝐚𝐫𝐭𝐞𝐝=========> https://bs786s.blogspot.com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button