Mwenge kukagua miradi ya Sh bilioni 23.8 Kagera

KAGERA: Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa amepokea Mwenge wa Uhuru kitaifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martini Shigella katika kijiji cha Nyakabango wilayani Muleba, Kagera.
Akipokea mwenge huo, RC Mwassa amesema kuwa mwenge huo utazindua kukagua kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo 53 yenye thamani ya Sh bilioni 23.8.

Alisema kuwa amesoma vipengere vya mwenge na kuvielewa vyema mwaka huu hivyo Mkoa wa Kagera uko tayari kutetea ushindi wake wa kitaifa wa mwaka Jana ambapo mkoa wa Kagera ulipata nafasi ya kwanza kitaita Tanzania Bara na Visiwani .
Mara baada ya kupokea mwenge huo alimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk Abel Nyamahanga na kuanza kukimbizwa wilayani Muleba ambapo umezindua na Kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.




