Mwenge wa Uhuru wawasili Geita

GEITA; MBIO za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 zimeingia rasmi mkoani Geita zikikitokea mkoani Mwanza Septemba 01, 2025, na ukiwa mkoani Geita Mwenge huo utakimbizwa kwenye wilaya tano za mkoa huo hadi Septemba 07, 2025.

Akizungumza mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella alisema mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Geita utakimbizwa umbali wa Km 653 katika halmashauri sita zenye jumla ya miradiĀ 61.



