Mwigulu: Waliopora mali za wananchi warudishe

WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amesema watu wote waliopora mali za wenzao ikiwemo ardhi warudishe wenyewe kabla hawajafikiwa na mkono wa serikali. Aidha, amewataka wananchi kutoa taarifa katika mamlaka zinazohusika pale wanapokutana na uonevu kwa kuwa serikali imedhamiria kutofanya ustaarabu kwa watu waonevu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kongamano la mwaka la wamachinga na madereva wa pikipiki na bajaji za kubeba abiria na kuwahakikishia kwamba serikali imeyapokea malalamiko yao kuhusu kuonewa wakati wakitekeleza majukumu yao. Amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeonesha mfano wa kusimamia haki na itaendelea kufanya hivyo ili watu waendelee kufanya kazi kwa uhuru kwa ajili ya maendeleo yao na ya nchi.
Ametoa baadhi ya mifano ya watu walioporwa haki zao akiwepo mama aliyemtaja kwa jina la Asha, Mkazi wa Dar es Salaam ambaye alinunua kiwanja chake tangu mwaka 2009 na miaka takribani 10 baadaye akaja mtu mwingine aliyesema amekinunua. Kutokana na mkasa huo, alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kufuatilia kisa cha mama huyo na kumtaka aliyemdhulumu arudishe haki ya mama huyo ndani ya siku saba kuanzia jana na kama hatofanya hivyo baada ya muda huo nyumba hiyo ibomolewe na mama huyo kurudishiwa nyumba yake.
Vilevile, Dk Mwigulu ameagiza wamachinga, madereva wa bodaboda na bajaji na mamalishe na babalishe wasifanyiwe uonevu wakati wa kutekeleza majukumu yao. Amesema ni lazima kuheshimu watu na kazi zao na kwamba yamekuwepo malalamiko kama vile ya masharti ya mikopo inayotolewa kwa ajili ya makundi hayo kuwa magumu kama kutaka hati ya nyumba, sharti ambalo ni ngumu watu waliopo katika makundi hayo kutimiza ili kupata mikopo.
Amesema serikali itashirikiana na Benki ya NMB ambayo ndiyo inaratibu mikopo hiyo kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia ili waweze kuifanyia kazi na kuachana na mikopo mikali zaidi. Aidha, Dk Mwigulu alisema kwa kuwa shughuli hizo zinahitaji maeneo yenye upatikanaji wa wateja aliwataka viongozi wao kutoa mapendekezo ya maeneo yanayofaa kufanya biashara zao ili serikali iweze kushughulikia mchakato wa upatikanaji wake.
“Mikoa yote washirikiane na viongozi wa makundi haya na kama yanawazidi walilete tulichakate tufanye maamuzi ili kurasimishwa shughuli zenu na kama eneo linalofaa linahitaji fidia lazima tuingie gharama, kupata maeneo yenye hadhi yatakayosaidia katika vita dhidi ya umasikini,” alisema. SOMA: Makalla awafikia bajaji, bodaboda
Ameongeza kuwa serikali imejipanga kurahisisha shughuli za wananchi badala ya kuwaongezea vikwazo visivyo vya lazima, akisisitiza kuwa kila ofisa wa serikali anatakiwa kutambua kuwa yupo kazini kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Amesema zimekuwa zikitokea nafasi za ajira nje ya nchi kwa madereva bodaboda, bajaji na hata teksi na kuzitaka wizara zinazohusika na utoaji wa nyaraka zinazowawezesha waliopata nafasi kusafiri kuwarahisishia michakato ili wafanikiwe.
“Wizara ya Kazi, Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi na Tamisemi, kuna fursa nyingi zinapokuja shirikianeni na haya mashirikisho ili matangazo yawafikie wahusika na wekeni wazi vigezo na watakaotaka na warahisishieni wapate nyaraka,” alifafanua.
Ameagiza pikipiki na bodaboda zisishikiliwe pindi wanapokuwa na makosa bali mhusika aandikiwe faini na kupewa muda wa kuilipa kama inavyofanyika kwa magari. Pia, aliagiza maofisa wa jiji kuacha kutoza faini madereva wa bodaboda na bajaji wanaposhusha abiria kwa kuwa dereva anakuwa hana lengo la kupaki bali kumshusha abiria na kuondoka jambo ambalo mara nyingi husababishwa na madereva hao kutokuwa na eneo maalumu la kushushia abiria




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Jobathome1.Com