Mwinyi: CCM kuboresha maisha ya wafanyabiashara

ZANZIBAR : MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imejipanga kufanya kazi ya ziada katika Awamu Ijayo ili kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali.

Akizungumza na makundi hayo leo tarehe 30 Septemba 2025 katika Soko la Kibanda Maiti, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk. Mwinyi alisema tayari michoro ya Soko la Kisasa la Kibanda Maiti imekamilika na fedha za kutosha zimetengwa ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali ijayo itaimarisha upatikanaji wa mikopo isiyo na riba kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, huku wale wanaoonyesha rekodi nzuri ya urejeshaji mikopo wakiongezewa fursa zaidi. Dk. Mwinyi aliwaomba wananchi kuendelea kuamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kumchagua yeye pamoja na wagombea wa chama hicho katika ngazi zote, ili kuweza kutekeleza kwa mafanikio ahadi zinazotolewa sasa.

Vilevile, amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuhakikisha CCM kinapata ushindi wa kishindo. SOMA: Mwinyi awaomba kura wauza samaki,wajasiriamali

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button