Nadal kukosa ‘Australia Open’

MCHEZAJI wa tennis, Rafael Nadal atakosa michuano ya Australian Open na badala yake atarejea Uhispania kwa ajili ya matibabu ya jeraha la nyonga.

Nadal ,37, alipata jeraha hilo kwenye michuano ya Kimataifa ya Brisbane hata hivyo alitegemewa huenda angeshiriki michuano hiyo itakayoanza kesho.

Mhispania huyo alirejea muda mrefu baada ya takriban mwaka mmoja nje ya uwanja kutokana na majeraha, akishinda mechi zake mbili za kwanza mjini Brisbane kwa seti za moja kwa moja.

Nadal alisema uchunguzi ulionesha kupasuka amepasuka kidogo kwenye misuli lakini sio katika eneo la jeraha lake la awali la muda mrefu.

Nadal ambaye hakuwa amecheza mechi yoyote kwa siku 349 kabla ya ushindi wake wa kwanza dhidi ya Dominic Thiem, alisema matokeo yalikuwa “habari njema” lakini akaongeza “hayuko tayari kushindana katika kiwango cha juu zaidi”.

“Nimefanya kazi kwa bidii sana katika mwaka huu kwa kurudi tena na kama nilivyotaja kila mara lengo langu ni kuwa katika kiwango changu bora katika miezi mitatu,” Nadal alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Habari Zifananazo

Back to top button