“Nasema Siondoki” William Ruto

KENYA : RAIS wa Kenya, William Ruto, amepinga vikali wito unaoendelea wa kumtaka ajiuzulu, akisema madai hayo hayana msingi.

Kauli hiyo ameitoa kufuatia ongezeko la nyimbo na kauli za ‘Ruto Must Go’ zinazotawala maandamano ya mitaani na mitandao ya kijamii.

Akihutubia katika Soko la Hisa la Nairobi (NSE) Jumatano, Rais Ruto alihoji sababu za shinikizo la kumtaka kuondoka madarakani kabla ya muda wake kumalizika. SOMA: Idadi ya vifo yaongezeka Kenya

“Kama wale waliokuwa kabla yangu, wakati wangu utafika na nitakwenda,” alisema. “Lakini, kwa heshima, mabwana na mabibi, sababu zenu ni zipi za ‘Ruto lazima aondoke’?”

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Kenya imeshuhudia maandamano makubwa yanayoongozwa na vijana wakilalamikia gharama kubwa ya maisha, ongezeko la kodi, ukosefu wa ajira, ufisadi serikalini pamoja na mageuzi ya sera za serikali yake ambazo zimezua upinzani mkali.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button