Nchi za Kiarabu,Kiislamu kujitenga na Israel

DOHA, QATAR : VIONGOZI wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu wamesema wanapitia upya mahusiano yao na Israel kufuatia shambulizi kubwa lililofanywa na nchi hiyo dhidi ya viongozi wa Hamas mjini Doha wiki iliyopita.

Tamko hilo limetolewa na viongozi wa takriban mataifa 60 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ile ya nchi za Kiislamu, baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura uliofanyika jana mjini Doha. SOMA: Doha yalaani matamshi ya Israel

Katika kikao hicho, viongozi hao wamesema kuwa mbali na kutafakari upya mahusiano ya kidiplomasia na Israel, mataifa wanapaswa pia kuchukua hatua za kisheria na kiutendaji kuzuia hujuma zaidi dhidi ya Wapalestina. Mashambulizi ya Israel mjini Doha yamelemaza juhudi za kidiplomasia zilizokuwa zikiongozwa na Qatar na Misri, ambazo ziliikuwa zinalenga kumaliza vita vya karibu miaka miwili katika Ukanda wa Gaza.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button