Nchimbi sasa kuwasha moto Njombe

NJOMBE : MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi ameanza rasmi kusaka kura za chama hicho mkoani Njombe leo Septemba 22, 2025, akianzia Jimbo la Ludewa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe, Julius Peter kesho Septemba 23, ataanza mapema asubuhi katika Jimbo la Wanging’ombe eneo la Igwachanya, kisha kuendelea Makete wilayani Iwawa na baadaye Njombe Mjini ambako atahutubia wakazi wa Jimbo la Njombe Mjini.

Safari ya kampeni mkoani humo itahitimishwa Septemba 24 ambapo atafanya mikutano katika Jimbo la Lupembe, eneo la Mtwango kuanzia saa 2:00 asubuhi, kisha kuelekea Makambako kwa mkutano mkubwa wa kampeni kabla ya kuondoka kuelekea mkoani Iringa jioni.

Kwa mujibu wa Peter, mikutano hiyo imelenga kutoa fursa kwa wananchi kumsikiliza mgombea mwenza huyo na kufahamu dhamira ya CCM katika kuendelea kuwatumikia Watanzania. SOMA: Dk Nchimbi: Mchagueni Samia aendeleze maajabu

Habari Zifananazo

23 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button