Ngajilo aahidi kushughulikia kero ya barabara na mfereji Isakalilo

Mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo (CCM), amesema kero kubwa inayowakabili wananchi wa Kata ya Isakalilo, hususan eneo la Mkoga, ni ubovu wa barabara ya Mkoga–Mgera yenye urefu wa kilometa 5.42, akiahidi kusimamia ujenzi wake mara baada ya kuchaguliwa.

Akihutubia wananchi wa kata hiyo leo, amesema barabara hiyo ni kiungo muhimu kitakachorahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa, hivyo kufungua milango ya biashara na kuinua uchumi wa wananchi wa eneo hilo.

Amesema pia serikali itashughulikia uboreshaji wa mfereji wa Mkoga, ili kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kinachoajiri wananchi wengi wa kata hiyo.

Pamoja na sekta ya kilimo, alisema masuala ya afya, elimu, maji na umeme yatapewa kipaumbele maalum.

Aliahidi pia kuimarisha vikundi vya kuweka na kukopa, pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata mikopo na vifaa vya kufanyia kazi kama vile vifaa vya kufugia nyuki na kutengeneza sabuni.

Kwa upande wake, mgombea udiwani wa Kata ya Isakalilo, Emanuel Mketo, amesema maendeleo ya mfereji huo ndiyo yalimvutia kugombea nafasi hiyo.

Amesema baada ya uchaguzi, atakaa pamoja na wananchi kupanga mikakati ya pamoja ya kuimarisha huduma za kijamii na kuibua fursa za uwekezaji katika kata hiyo yenye ardhi na mazingira rafiki kwa maendeleo ya kiuchumi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button