Ngajilo achanja mbuga, wapinzani wakijikongoja

IRINGA: Kampeni za uchaguzi jimbo la Iringa Mjini zimezidi kupamba moto, huku mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fadhili Ngajilo, akionekana “kuchanja mbuga” kata kwa kata, wakati wapinzani wake wakionekana kujikongoja kufikisha ujumbe wao kwa wapiga kura.
Wagombea wengine katika jimbo hilo ni pamoja na Chiku Alfan Wabwo (ACT), Ahmed Adam Lyellu (CUF), Hebron Lucas Kileta (NCCR), Shukran Peter Mtuli (DP), Christian Thomas Mbalinga (NRA) na Masasi Daud Issa (ADC).
Ngajilo, ambaye ameahidi kufanya miaka mitano ijayo kuwa ya mafanikio na maendeleo ya kweli, leo katika kata ya Mtwivila amewataka wananchi kumpa ridhaa ili aweze kushughulikia changamoto zao za muda mrefu.
“Mimi si mtu wa kushindwa. Maombi ya wananchi wa Kata ya Mtwivila tutayatekeleza. Kuanzia sekta ya elimu, miundombinu hadi huduma za afya — ndani ya siku 100 tutaanza kuona mabadiliko,” alisema Ngajilo.
Kuhusu changamoto za mikopo kandamizi, Ngajilo amesema serikali itapambana na wakopeshaji “kausha damu” na kuweka mfumo wa mikopo yenye heshima kwa wajasiriamali.
Kwa upande wa usalama, amewahakikishia wananchi wa Mtwivila kuwa ataweka mikakati ya kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha raia na mali zao zinalindwa, huku akiweka msisitizo juu ya amani na mshikamano.
Akiwaomba wananchi kuunga mkono ajenda ya viwanda, Ngajilo alikumbusha historia ya Iringa kuwa mkoa wa viwanda miaka ya 1990, akitaja viwanda vya Cotex, SIDO, Motor Mark, Tobacco na Coca-Cola kuwa mfano wa uchumi uliokuwa imara.
“Ilani ya CCM ukurasa wa 15 imezungumzia kuanzishwa kwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Nitapambana viwanda hivyo vije Iringa, maana bila mzunguko wa fedha biashara hufa,” alisema.
Ngajilo pia amegusia sekta ya madini kama eneo jipya la fursa kwa wananchi wa Iringa, akisema ni wakati wa kuitumia sekta hiyo kubadilisha maisha ya watu.
Ameongeza kuwa safari ya kuifanya Iringa kuwa jiji ni ndefu, na kwamba ni muhimu baadhi ya maeneo ya vijijini kuingizwa rasmi katika mipaka ya mjini ili kunufaika na fursa za kimaendeleo.
“Tunahitaji oparesheni ya kuboresha majengo yetu. Mji uwe wa kisasa, wa mfano, wenye makazi bora na mazingira safi,” alisisitiza.
Katika mkutano huo, makada wa CCM walimwagia sifa wakimtaja kama kijana msomi mwenye shahada mbili, mwalimu wa sekondari na vyuo vikuu, mwenye uwezo mkubwa wa hoja na uadilifu.
“Kama ameweza kufundisha wasomi, atashindwaje kupeleka hoja bungeni?” alisema aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa, IbrahimNgwada.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com