Ngajilo ataja fursa mpya za kilimo na ufugaji

IRINGA: Mgombea ubunge wa Iringa Mjini, Fadhil Ngajilo, amesema wakati umefika kwa wananchi wa Iringa mjini kutumia ardhi ndogo walizonazo kuendesha kilimo na ufugaji wa majumbani wenye tija, vitakavyoweza kubadilisha maisha yao na kuchangia uchumi wa mji huo.

Akizungumza na wakazi wa kata ya Ruaha katika mfululizo wa kampeni zake, Ngajilo alisema si lazima mtu awe na shamba kubwa ili awe mkulima au mfugaji wa kibiashara, kwani teknolojia ya sasa inaruhusu kufanya kilimo katika maeneo madogo majumbani na kupata matokeo makubwa.

“Elimu ya ujasiriamali kwenye kilimo ndiyo hoja yangu kubwa. Tunataka tutoke kwenye kilimo cha kujikimu, twende kwenye kilimo cha biashara. Sio lazima ukalime mbali — unaweza kulima nyumbani, ukavuna vizuri na kuuza,” alisema.

Ameeleza kuwa serikali na wadau watasaidia wananchi kupata teknolojia za kilimo cha kisasa, ikiwemo kilimo cha mboga mboga, matunda, na ufugaji wa kuku, sungura, na samaki katika mabwawa madogo ya nyumbani.

“Tuache kufikiria kuvua samaki Bwawa la Mtera pekee. Tunaweza kutengeneza mabwawa madogo majumbani na ikawa biashara kubwa. Serikali ina mipango ya kuzalisha vifaranga vya samaki vitakavyosaidia miradi hii,” alifafanua.

Ngajilo alisema zaidi ya asilimia 31 ya wakazi wa Iringa ni wakulima na asilimia 33 ni wajasiriamali, hivyo anapanga kusimama bega kwa bega nao kuhakikisha wanapata elimu ya biashara na masoko.

Aidha, Ngajilo alisisitiza umuhimu wa kuunganisha biashara ndogo ndogo na taasisi za mikopo ya teknolojia, akisema ni njia sahihi ya kukuza uchumi wa mji huo.

“Tunataka biashara ndogo zikue,” alisema na kutolea mfano wa biashara ya bagia ambayo ni maarufu Iringa, inavyoweza kusafirishwa hadi Dodoma na Dar es Salaam katika masoko makubwa zaidi.

Akigusia sekta ya viwanda, Ngajilo alisema atapaza sauti bungeni kuhakikisha Iringa inapata viwanda vya kimkakati kama vya mbolea na vya kuchakata mazao ya kilimo, hususan katika eneo la Kibwabwa, lililotajwa kuwa kitovu cha kongani ya viwanda vidogo.
“Tunahitaji viwanda virejee Iringa ili kuimarisha zaidi uchumi wa Iringa,” alieleza.

Mbunge huyo pia aligusia michezo kama eneo jingine la ajira na afya, akiahidi kwamba ndani ya miaka mitano, Iringa itakuwa na ligi kuu yake, huku akinamama wakishiriki michezo ya lede kwa ajili ya afya na kipato.

“Michezo ni uchumi. Kuna mabilionea katika michezo. Iringa itasonga mbele tukitumia vipaji vyetu vizuri,” alisema Ngajilo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button