NGAJILO: Nitafanya Iringa uwe mji wa biashara

Mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fadhili Ngajilo, amesema dhamira yake ni kuona mji wa Iringa unakuwa kitovu cha biashara na ajira endelevu kwa wananchi wa kada zote, hususan vijana na wanawake.
Akizungumza leo katika Mtaa wa Kihodombi A, Kata ya Isakalilo, Ngajilo ambaye ameendesha mikutano saba katika kata hiyo ndani ya siku moja, alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imeweka msingi mzuri wa uchumi wa watu, na jukumu lake kama mbunge litakuwa ni kuimarisha jitihada hizo kupitia mikopo yenye riba nafuu na upatikanaji wa vifaa vya ujasiriamali.
“Tunataka Iringa iwe mji wa biashara. Mikopo iwe na utu kama kauli mbiu ya Rais — Kazi na utu. Tutaunganisha wajasiriamali na taasisi za kifedha ili wapate mikopo ya vifaa, mashine na elimu ya ujasiriamali. Bila elimu ya biashara huwezi kusonga mbele,” alisema Ngajilo.
Akiendelea kuzungumza mbele ya mamia ya wakazi wa Kihodombi, Ngajilo aliahidi kuanzisha vikao vya mara kwa mara na wafanyabiashara wadogo mara baada ya uchaguzi, likiwemo kundi la wauzaji wa pombe za kienyeji.
“Baada ya uchaguzi nitakuwa na vikao na wafanyabiashara wa pombe za kienyeji. Wengi wao wanapata manyanyaso ya muda wa kufunga mapema. Sipendezewi na hilo, kwa sababu biashara hiyo imelea watu wengi wapo waliokuja kuwa maprofesa, wanajeshi, na polisi. Nitasimamia haki yenu mfanye biashara kwa heshima na upendo,” aliongeza.
Ngajilo alisema dhamira yake ni kubadilisha maisha ya watu wa Iringa kupitia uchumi shirikishi unaotegemea elimu ya ujasiriamali, mikopo yenye masharti nafuu, na ushirikiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi.
“Nitakuwa nanyi mara nyingi, nikisikiliza changamoto zenu na kuzifikisha sehemu husika ili zitatuliwe kwa wakati. Najua kero zinazowagusa vijana, kina mama, watoto na wazee — tutashughulika nazo kwa vitendo,” alisema.
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com