Ngajilo: Nitapanda meza bungeni kupigania huduma za kibingwa Iringa

Mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fadhili Ngajilo, amesema moja ya ajenda zake kuu bungeni itakuwa ni kuhakikisha huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo na saratani zinapatikana kwa kudumu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, ili wananchi wa Nyanda za Juu Kusini wasilazimike tena kusafiri hadi Dar es Salaam au Dodoma kwa matibabu hayo.
“Nataka huduma hizo ziwe za kudumu hapa Iringa. Wagonjwa wa moyo na saratani kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wapate matibabu bora bila kulazimika kwenda mbali. Nitapanda meza bungeni, nitaruka sarakasi kama itahitajika, kuhakikisha huduma hizo zinakuwepo hapa,” alisema Ngajilo kwa msisitizo.
Ngajilo aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mlandege, ambapo pia alizungumzia hali ya masoko ya Mwamwindi na Mlandege, akiahidi kushirikiana na wafanyabiashara ili kufufua shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
“Kuna soko zuri sana la Mwamwindi, limejengwa kwa gharama kubwa, lina historia kubwa, lakini leo limepooza, milango imefungwa, biashara haziendi. Hilo soko halijatendewa haki. Tunapaswa kukaa na wafanyabiashara, kuelewa changamoto zao na kulihuisha upya,” alisema Ngajilo.
Soko la Mwamwindi lilijengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 2.5, likiwa na miundombinu ya kisasa ikiwemo vizimba vya wafanyabiashara, mifumo ya maji, umeme na vyumba vya kuhifadhia bidhaa.
Hata hivyo, kutokana na changamoto za usimamizi na ukosefu wa mpango jumuishi wa biashara, soko hilo limeendelea kuwa butu kwa muda mrefu na halijarejesha thamani ya uwekezaji uliowekwa.
Ngajilo alisema pamoja na mpango wa kulifufua soko hilo, CCM inaona umuhimu wa kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali kwa elimu na mitaji midogo, hasa kupitia taasisi zinazotoa mikopo kwa riba nafuu.
“Mlandege ni eneo la biashara kubwa. Tutawaunganisha na taasisi zinazotoa mikopo nafuu, lakini zaidi tuwape elimu ya ujasiriamali wajue maana halisi ya kujiajiri. Lazima tuondokane na fikra za kutegemea ajira; tuelekee kwenye kujiajiri na kuzalisha kipato,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa, Said Rubeya, aliwataka wananchi wa Iringa kuendelea kuiamini CCM, akisema chama hicho ndicho pekee chenye uwezo na dhamira ya kutekeleza kwa vitendo Ilani yake ya Uchaguzi.
“Chagueni CCM, tutatekeleza Ilani hii kwa kishindo. Tumetekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, na tutaendelea kufanya zaidi,” alisema Rubeya.
Rubeya alisema Ilani ya CCM 2025-2030 itazidi kuzingatia mageuzi ya kiuchumi, hasa katika sekta za biashara, afya, na ajira, ili kuhakikisha wananchi wa Iringa wananufaika moja kwa moja na uwekezaji wa serikali.
Make money while staying at home and working online. I just received $23,783 for my work last month, and I was doing this part-time. This year, I plan to earn even more, and I believe you can also make extra cash from this job. To join right now, follow the details on this website.
Open This… http://Www.Work99.Site
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com