Ni zamu ya Manara kuishika Dar kesho

DAR ES SALAAM; MGOMBEA udiwani wa Kata ya Kariakoo, Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Haji Manara kesho Septemba 11, 2025, anatarajia kuzindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na DailyNews Digital, Manara amesema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu.

“Wana CCM, wananchi wa Kata ya Kariakoo na Wakazi wa Dar es Salaam na wale Friends of Manara tukutane maeneo ya Mtaa wa Mkunguni na Nyamwezi kuanzia saa 5 asubuhi. Utakuwa uzinduzi wa aina yake.

“Utakuwa uzinduzi wa aina yake, nawakaribisha wote mje mshuhudie tukio letu,” amesema Manara ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania pekee aliyeongoza kwa nyakati tofauti Idara za Habari za miamba ya soka nchini Simba na Yanga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button