‘NIDA inaondoa vikwazo huduma za msingi’

DAR ES SALAAM: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewahimiza wananchi kujisajili katika mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili waweze kunufaika kikamilifu na huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia mifumo iliyounganishwa na mamlaka hiyo.
Katambi ametoa wito huo wakati wa ziara yake ya kwanza katika ofisi za NIDA tangu ateuliwe kushika wadhifa huo, akisema usajili wa NIDA ni nyenzo muhimu inayowawezesha wananchi kutambuliwa kwa urahisi na kupata huduma kwa haraka katika taasisi za umma na binafsi.
Amesema Kitambulisho cha Taifa kinarahisisha upatikanaji wa huduma nyingi muhimu ikiwemo huduma za afya, elimu, umeme, maji, benki, hati za kusafiria, leseni za udereva na biashara, utambulisho wa mlipa kodi (TIN), usajili wa kampuni binafsi pamoja na huduma za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

“NIDA inaondoa vikwazo kwa wananchi wanapohitaji huduma za msingi na hivyo kuchangia ufanisi katika utoaji wa huduma mbalimbali,” amesema Katambi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema zoezi la kushughulikia changamoto za majina kwa wananchi wenye sababu na vielelezo stahiki linaendelea nchini kote.

Amesema hatua hiyo inahusisha pia wananchi waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ulioruhusu kurekebishwa kwa taarifa zao katika mfumo wa NIDA ili ziendane na majina yao halisi, badala ya majina yaliyokuwa yameandikwa katika vyeti vya elimu vilivyogushiwa katika ngazi mbalimbali.
Kaji amewahimiza wananchi ambao bado hawajachukua vitambulisho vyao katika ofisi za NIDA za wilaya kwenda kuvichukua ili waanze kunufaika na matumizi yake katika kupata huduma mbalimbali.




I earned $17,932 last month by working online for just 2 hours a day. This job is simple, flexible, and beginner-friendly,S1 making it accessible to everyone. It has helped me manage my finances effortlessly while focusing on my education as a full-time student.
You can click on this the website and begin
right away….www.today.earn54.com