Niffer, wengine waachiwa huru

DAR ES SALAAM: MFANYABIASHARA Jennifer Jovin (26) maarufu ‘Niffer’na mwenzake waliokouwa wakikabiliwa na kesi ua uhaini wameachiliwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kueleza hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Mika Chavala ambao wikuwa ni miongoni mwa washitakiwa 22 katika kesi namba 26388 ya mwaka 2025 ambao 20 kati yao walifutiwa mashitaka yao Novemba 25,mwaka huu.
Hatua hiyo imefikiwa leo Desemba 3,2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati shauri hilo lilipopelekwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya kwa ajili ya kutajwa.
Awali, Wakili wa Serikali, Titus Aron alidau shauri hilo lilipelekwa kwa ajili ya kutajwa, lakini DPP kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 92(1) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai CPA hana nia ya kuendelea kuwashitakibwashitakiwa wote wawili.

“Hivyo kwa mamlaka hiyo aliyoanayo chini kifungu tajwa ameamua kuwaondolea mashitaka washitakiwa wote wawili,” alidaiTitus.
Baada ya kuelezwa hayo Wakili wa Utetezi, Peter Kibala alidai wamesikia na hawana pingamizi katika hilo kwakuwa ndiyo sheria inavyoelekeza, hivyo alidai anaiomba mahakama iweze kutamka kwamba washitakiwa wameachiwa.
Hakimu Lyamuya aliwaeleza washitakiwa kuwa upande wa mashitaka umewasilisha ombi ya kuwafitia mashitaka chini ya kifungu kilichotajwa, hivyo Mahakama inakubali ombi hilo na kueleza imewaachia huru washitakiwa isopokuwa kama watashikiliwa kwa jambo jingine.
Washitakiwa hao wanakuwa ni miongoninwa wsshitakiwa 1736 wanaoondolewa mashitaka na kuachiwa kati ya 2045 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhaini mahakamani kutokana na vurugu ziliotokea Oktoba 25,mwaka huu.
Washitakiwa hao wameachiwa kufuatia msamaha wa Rais Samia Suluhu Hassan alioutoa Novemba 13,2025 wakati akihutubia Bunge mkoani Dodoma kwa mara ya kwa baada ya serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani.



