‘Nimewajengea heshima wananchi Kigoma’

KIGOMA; Mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma mjini Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa miaka 15 ambayo amekuwa mbunge katika majimbo mawili ya Mkoa Kigoma amejenga heshima kwa wananchi wa mkoa huo na sasa wanatembea na kuona fahari kutangaza wanatoka Kigoma.
Zitto amesema hayo akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma na kusema kuwa amejenga heshima na utu kwa watu wa mkoa Kigoma na kujiona kuwa sasa siyo raia daraja la pili.
Amesema pamoja na kujenga kujiamini na kuwafanya kuwa watu wanaojenga hoja, pia kwa maisha yake ya siasa amepigania changamoto ya watu wa mkoa huo kuonekana siyo raia, akitaka uwepo wa usawa katika jambo hilo kama inavyofanywa mikoa mingine ambayo inapakana na nchi jirani.
Akieleza miaka mitano aliyokuwa mbunge jimbo la Kigoma Mjini (2015 – 2020) alisema kuwa kwa kusaidiana na idadi kubwa ya madiwani na meya waliokuwa nayo, walifanya kazi kubwa ikiwemo kuimarisha barabara za manispaa ya Kigoma Ujiji, kuimarisha biashara kwa kujenga masoko na kuanzisha miradi ambayo imekuwa ni chachu kubwa ya kujenga uchumi wa wananchi wa manispaa hiyo.
Katika hilo alisema kuwa wametengeneza mabango na kusambaza mji mzima, kuonesha ushahidi ili wasionekane waongo hivyo alitaka mwenye hoja anayepinga maneno yake aoneshe kwa vitendo kwa ushahidi.
Awali mgombea mwenza wa urais wa ACT Wazalendo, Fatma Fereji alisema kuwa wananchi wa jimbo la Kigoma Mjini watafanya kosa kubwa na ambalo watalijutia kama hawatamchagua Zitto Kabwe, kwani amekuwa mtetezi mkubwa wa mambo yanayogusa maisha yao.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com