Nishati watoa elimu nishati safi ya kupikia

TANGA: Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake imeendelea kutumia njia mbalimbali kufikisha elimu ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi ambapo safari hii elimu hiyo inatolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya Usagara jijini Tanga.

Akizindua Maadhimisho hayo leo jijini Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Burian ameipongeza Wizara ya Nishati na taasisi zake kwa kushiriki maadhimisho hayo yanayotarajiwa kumalizika Oktoba 16 mwaka huu.

Dk. Burian ameeleza kuwa nishati safi ya Kupikia ina mchango wa moja kwa moja katika suala la chakula kwani Serikali kwa sasa inahimiza matumizi ya nishati safi katika kupikia chakula.

Aidha, akiwa katika Banda la Wizara ya Nishati, Dk. Burian alielezwa na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Omari Khalifa kuwa, Wizara ikishirikiana na taasisi zake, inatekeleza ajenda ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia ambayo kinara wake ni. Rais, Dk Samia Suluhu Hassan.

Khalifa amesema katika maadhimisho hayo Wizara ya Nishati kupitia taasisi yake ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kuuza majiko takriban 500 ya Gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya Sh 17,500/= kwa wakazi wa Tanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la kufikia asimilia 80 ya wananchi wanaotumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  2. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button