NLD kuunganisha vijiji 5,000 maji ya bomba

DAR-ES-SALAAM : CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kimesema serikali yake itaunganisha zaidi ya vijiji 5,000 kwenye huduma ya maji ya bomba kufikia mwaka 2030.
Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya NLD 2025-2030, chama hicho pia kitajenga visima virefu, mabwawa ya maji ya mvua na vituo vya kuchotea maji karibu na makazi ya wananchi. Aidha, NLD imeahidi kulinda na kurejesha vyanzo vya maji vya asili kupitia sheria na elimu kwa jamii.
Nishati
Ilani imeeleza NLD itapanua huduma ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA) hadi vijiji vyote vilivyobaki ndani ya miaka mitano. Pia itajenga vituo vya umeme wa jua, upepo na maji, huku wananchi wakipatiwa vifaa vya nishati mbadala kwa mikopo nafuu.
Mazingira
NLD imeahidi kupiga marufuku ukataji wa misitu bila kibali na kupanda miti milioni 100 ndani ya miaka mitano. Pia itarasimisha biashara ya mkaa kwa teknolojia rafiki na kuingiza elimu ya mazingira katika mitaala ya shule. SOMA: NLD yaahidi elimu bure hadi vyuo vya kati