NLD yaahidi elimu bure hadi vyuo vya kati

DODOMA: CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kimesema serikali yake itatoa elimu bure hadi kidato cha sita na vyuo vya kati vya umma.
Ilani ya uchaguzi ya chama hicho 2025-2030 imeeleza kwamba serikali hiyo itaweka mfumo wa kusaidia gharama za chuo kikuu kupitia mikopo nafuu yenye uangalizi wa haki. NLD inaeleza itabadili mitaala ya msingi, sekondari na vyuo ili izingatie ujuzi wa karne ya 21, teknolojia, ubunifu, maarifa ya fedha, lugha za kigeni na masuala ya mazingira.
Ilani hiyo inaeleza kwamba chama hicho kitaanzisha mfumo wa elimu ya kidijiti shuleni na kupanua miundombinu na idadi ya vyuo vya Veta hadi katika kila kata. NLD itawezesha ushirikiano kati ya Veta, Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na sekta binafsi kutoa mafunzo yenye tija itajenga madarasa, mabweni, maktaba na maabara katika shule zote. SOMA: Kumekucha kampeni za Uchaguzi Mkuu