NLD yaja na mfumo bima ya afya kwa wote

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo amesema serikali yake itapunguza posho za wabunge na kuongeza mishahara ya watumishi wa serikali.
Doyo alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika eneo la Soko Kuu la Chifu Kingalu katika Manispaa ya Morogoro.
Alisema pia serikali yake itaboresha huduma za afya na itaanzisha mfumo wa bima ya afya kwa wote (NHIS).
Doyo alisema kupitia mfumo huo, kila Mtanzania atakuwa na fursa ya kupata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia bima hiyo na pia itafidia watu wasio na uwezo kupitia mfuko wa afya ya jamii.
Alisema serikali yake pia itaongeza bajeti ya ununuzi wa dawa na vifaatiba hadi angalau asilimia 20 ya bajeti ya sekta ya afya na kuanzisha mfumo wa usambazaji wa dawa wa kitaifa kwa kidijiti ili kuhakikisha dawa zinafika kwa wakati vituoni.
Alitaja eneo lingine ni kuongeza watumishi wa afya kwa kutoa ajira mpya za madaktari, wauguzi na wahudumu wa afya kwa kuzingatia uwiano wa kimataifa, kutolewa kwa mafunzo mara kwa mara na motisha kwa wanaofanya kazi vijijini.
Doyo alisema kupaumbele kingine ni kwenye uboreshaji miundombinu ya vituo vya afya, kuimarisha huduma za kinga na elimu ya afya
Alisema serikali ya NLD itatumia rasilimali za taifa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania ili kwenda kuboresha maisha yao kupitia rasilimali zinazozunguka wananchi ili maisha yao yawe mazuri.
Doyo alitaja eneo lingine la kipaumbele kwenye ilani ya chama hicho ni kutoa elimu bora na bure ngazi zote na kuweka mfumo wa kusaidia gharama za chuo kikuu kupitia mikopo nafuu yenye uangalizi wa haki.
Alisema ilani hiyo imeeleza namna ya kuboresha mitaala ili kulingana na mahitaji ya soko, kukuza elimu ya ufundi na ujasiriamali, kuboresha miundombinu ya shule, kuwajengea walimu uwezo, upatikanaji wa elimu jumuishi kwa makundi maalumu.
Doyo aitaja kipaumbele kingine kwenye ilani hiyo ni suala la ujenzi wa barabara za kisasa zenye njia mbili na zaidi katika barabara ya Segera – Arusha, Segera – Chalinze, Chalinze – Morogoro- Tunduma.
Alisema barabara ya Morogoro- Chalinze – Tunduma ni kuifanya kuwa ya njia mbili ili kuwezesha kuhudumia mizigo ya kimataifa, kupunguza msongamano, ajali na kuimarisha uchumi wa mikoa ya kati na Kusini.
Doyo aliwasihi Watanzania waendelee kudumisha amani na kwa waliojiandikisha kupiga kura Oktoba 29, mwaka huu wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kumchagua yeye ili awe rais wao kwa ajili ya maendeleo yao.
Naye mgombea ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya NLD, Halima Habibu alisisitiza kudumisha amani kwa kuwa ni msingi wa maendeleo.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com