MAREKANI : WAENDESHA mashtaka nchini Marekani wamesema nguli wa miondoko ya muziki wa Rap na mtayarishaji wa muziki Sean Diddy Combs anavunja sheria za gereza kwa kuwasiliana na mashahidi wa kesi yake kinyume cha sheria.
P DIddy anashutumiwa kwa kushawishi mashahidi kwa kutumia simu za wafungwa wengine huku akiendelea kutumia simu za watu wengine ambazo haziko kwenye orodha ya mawasiliano iliyoidhinishwa.
Waendesha mashitaka wamesema katika jalada la mahakama kuwa, uhakiki wa simu zilizorekodiwa pia wamegundua Combs aliagiza familia yake kuwasiliana na mashahidi watarajiwa kabla ya usikilizwaji wa kesi yake.
Pia walinukuu ujumbe wa Instagram uliotumwa na mwanamke, anayepinga madai yaliyotolewa na mwimbaji Dawn Richard katika kesi dhidi ya Combs.
Waendesha mashitaka wanadai taarifa ya mwanamke huyo iliandaliwa na Combs wakati wa mawasiliano kwa ujumbe mfupi na simu nyingi kutokea gerezani.
Pia wanadai kulikuwa na mwelekeo wa wazi kwamba Combs alimlipa mwanamke huyo, baada ya kuchapisha ujumbe wake.
Combs mwenye umri wa miaka 55 kwa sasa yuko kizuizini huko Manhattan na ameendelea kukana mashtaka yake dhidi ya kesi inayomkabili .
SOMA: P Didy akutana na kesi mpya 120