Marekani yaidhibiti Pareco-FF

WASHINGTON DC : MAREKANI imeliwekea vikwazo kundi lenye silaha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linaloshutumiwa kwa uchimbaji haramu wa madini.

Washington imetangaza kuzuia mali za kundi linalofahamika kama Coalition des Patriotes Resistants Congolais-Forces de Frappe (Pareco-FF), kikundi chenye silaha kinachopambana pia na M23.

Aidha, kampuni ya uchimbaji madini ya Congo na makampuni mawili ya Hong Kong yamewekewa pia vikwazo kwa tuhuma za kununua madini kutoka kwa kundi hilo lenye silaha.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Tammy Bruce amesema kuwa Marekani inatuma ujumbe ulio wazi kuwa hakuna kikundi chenye silaha au taasisi ya kibiashara isiyoweza kuwekewa vikwazo ikiwa vitachangia kuvuruga amani, utulivu na usalama nchini Congo.

Kundi la Pareco-FF lina ushawishi mkubwa huko  Rubaya , mashariki mwa DRC, kunakochimbwa kati ya asilimia 15 na 30 ya madini ya Coltan kote duniani, ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki kama vile kompyuta na simu za mkononi.

SOMA: Rwanda, DRC waanza kutekeleza makubaliano ya amani

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button