Pazia kampeni lafungwa leo

MWANZA; VYAMA vya siasa vinahitimisha leo siku 60 za kampeni za Uchaguzi Mkuu ambazo zimetajwa kuandika historia kwa kuwa zenye amani na utulivu.
Kati ya vyama 18 vinavyoshiriki uchaguzi huo kesho vilivyoanza kampeni Agosti 28, kulingana na ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), 17 ndivyo vyenye wagombea wa nafasi ya urais.
INEC inasimamia uchaguzi huo wa saba wa vyama vingi kwa kuzingatia Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 2024.
Baadhi ya vyama, kikiwemo cha ADA TADEA, NCCR Mageuzi na NRA vilimaliza kampeni za wagombea urais jana.
Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mgombea wake wa urais, Samia Suluhu Hassan anahitimisha kampeni zake leo jijini Mwanza.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenan Kihongosi alisema Mwanza jana kwamba Watanzania wanaendelea kuwa na matumaini na chama hicho.
Kihongosi aliwaeleza wahariri na waandishi wa habari kwamba CCM ina ilani bora ya uchaguzi inayogusa maslahi ya kila kundi kwenye jamii.
Alisema Ilani ya CCM ya 2025/2030 inaingia hadi ngazi ya familia, inatoa majibu ya maswali katika suala la maendeleo na kwamba Samia atawakomboa Watanzania kiuchumi.
Kihongosi alisema CCM itaendelea kufanya mambo makubwa kwa Watanzania ikiwemo kuzalisha ajira na ustawi wa jamii, kuwa suluhisho kubwa katika masuala ya afya na kuakisi mapinduzi ya kiuchumi na uzalishaji.
Alisema Samia anaijenga Tanzania ambayo rasilimali zake kuanzia ngazi ya wilaya hadi mikoa zinaongezwa thamani ili kufungua fursa kubwa za kiuchumi.
“Ni pamoja na serikali kuanzisha kongani za viwanda ili kuongeza thamani za mazao mbalimbali ya shambani. Hii itamkomboa Mtanzania kwa kumuwezesha auze bidhaa badala ya malighafi, hatimaye kuimarisha kipato chake,” alisema Kihongosi.
Alisema serikali ya CCM itaanzisha gridi ya taifa ya maji, itazalisha umeme zaidi ya megawati 8,000 kiasi ambacho ni mara mbili ya kinachozalishwa sasa.
Kihongosi alisema sekta binafsi itaongezewa nguvu kwa kuhakikisha kilimo kinakuwa juu ili Tanzania ilime na kufuga kisasa.
Alisema serikali ya CCM inawahakikishia wakulima upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati zikiwemo mbegu bora ili Tanzania iendelee kuwa na usalama wa chakula na akiba ya kuuza nje ya nchi.
“Sekta ya madini nayo itaboreshwa zaidi, lakini pia serikali kukuza makazi ya wananchi kwa ujenzi zaidi wa miundombinu ili kila kona ya nchi ifikike kwa urahisi. Kwa msisitizo ni kwamba ilani ya chama imegusa kila eneo, na huo ndio upekee wa Chama Cha Mapinduzi,” alisema Kihongosi.
Alisema Samia ameendelea kuwapa matumaini Watanzania kwa kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa kwa wakati.
Alitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP), Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo- Busisi), Reli ya Kisasa (SGR) na ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza.
Kihongosi alisema serikali ya CCM imefanya uboreshaji katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa walimu takribani 39,000 katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia.
“Na imeahidi ajira nyingine 7,000 kwa walimu endapo atapewa (Samia) ridhaa ya kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu unaofanyika kesho,” alisema.

Mafanikio kampeni
Kihongosi alisema zaidi ya mikutano 114 ilifanywa na mgombea huyo nchi nzima na kuhudhuriwa na watu wapatao milioni 25.
Alisema pia alisimama njiani na kusikiliza mahitaji ya wananchi ili ayatafutie ufumbuzi kila msafara wake uliposimamishwa hali inayoakisi tumaini kwa wananchi kwamba serikali yao inaendelea kuwajali.
“Aliunda pia kamati maalumu kupitia ofisi yake ili kila mwananchi mwenye jambo lake asikilizwe,” alisema Kihongosi.
Alisema katika kipindi chote cha kampeni Samia alinadi ilani ya chama kwa kuendeleza maelewano na mshikamo katika jamii ili kuwajengea matumaini mapya Watanzania kutokana na huduma ya kazi na utu ambayo CCM itawapatia kupitia serikali anayokwenda kuiunda atakapochaguliwa.
Kihongosi alisema kampeni hizo zimekuwa za mafanikio kwa kuwa takwimu zimeonesha watu zaidi ya milioni 57.1 wamefuatilia mikutano hiyo kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ndani na nje ya Tanzania.
Alisema namba za mitandao zimeonesha Samia amefuatiliwa mara milioni 164.9 na kwamba ni tafsiri ya kukubalika kwa uongozi wake unaojali utu kupitia matokeo aliyoonesha kwa wananchi.
Wakati huo huo, miongoni mwa watu wa kada tofauti wakiwemo wachambuzi wa masuala ya siasa waliozungumza hivi karibuni, walieleza upekee wa kampeni hizo zinazohitimishwa kwamba ni kuendeshwa kwa amani, utulivu na mshikamano miongoni mwa vyama tofauti na uzoefu wa vipindi vilivyopita.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com