PICHA: Wakuu wa divisheni na vitengo mafunzoni Urambo

BAADHI ya picha za matukio wakati mafunzo maalumu ya uhuishaji wa mpango mkakati wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa Wakuu wa Divisheni na Vitengo yakiendelea kwa wakuu wa divisheni na vitengo.

Mafunzo hayo yanaendelea kufanyika ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwake Desemba 16 na kutolewa na wataalamu kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Dodoma.

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Urambo inahuisha mpango mkakati wake ili kuboresha na kuhakikisha inatengeneza mazingira mazuri ya utendaji kazi unaopimika ili kwenda sambamba na sera, mipango na mikakati ya Kitaifa, Kikanda na Kidunia katika utekelezaji wa shughuli zake.

Ikumbukwe kuwa mafunzo ni msingi wa utendaji kwa mtumishi wa umma na huongeza chachu ya ufanisi kupitia mambo mbalimbali anayopata kupitia mafunzo hayo.

Mafunzo haya yanatarajia kuwa endelevu ili kuitengeneza Urambo bora na kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.



