Pinda mambo magumu ubunge CCM
DODOMA — Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtema aliyekuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Ardhi, Geophrey Mizengo Pinda, na kumteua Laurent Deogratius Luswetula kugombea ubunge wa Jimbo la Kavuu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Pinda, ambaye ni mbunge wa sasa wa Kavuu, alishindanishwa na wagombea wengine watatu ambao ni Laurent Deogratius Luswetula, Dama Samora Lusangija na Prudenciana Wilfred Kikwembe.



