Pole sana Rais

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole nyumbani kwake Ikulu Migombani kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali John Jacob Mkunda kufuatia kifo cha baba yake mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Ali Hassani Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29, 2024, Dar es Salaam na kuzikwa Machi 2,2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja.