Polisi Kagera yapokea kesi 279 ukatili, unyanyasaji

JESHI la Polisi mkoani Kagera limepokea kesi 297 za ubakaji kwa kipindi cha mwezi January hadi Desemba mwaka huu.
Hatua hiyo ni katika kuhakikisha linapambana na maswala ya ukatili na unyanyasi wa watoto wadogo na wanawake.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Brasius Chatanda amesema kuwa kesi nyingine za ukatili ni 22 za ulawiti, kesi 24 za mauaji ya watoto wadogo kikatili na kati ya hizo kesi 149 zimefikishwa mahakamani na kesi 148 zipo chini ya upelelezi ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wa kesi hizo.
Amesema kuwa jumla ya kesi 22 za ubakaji watuhumiwa 6 wamehukumiwa kifungo cha maisha jela watuhumiwa 16 wamepata kifungo cha miaka 30 jela, pia watuhumiwa 8 wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kesi za ulawiti, kesi nyingine 14 ziliwahusisha watoto wadogo chini ya miaka 14 ambao wamehukumiwa adhabu kwa mujibu wa sheria kama kuchapwa vibiko, kupewa onyo na kesi nyingine nne wamehukumiwa miaka 20 jela.
“Tumekuwa na ushirikiano mzuri na jamii ingawa bado Kuna mapungufu katika maswala ya Ubakaji mfano baadhi kuchelewa kutoa taaarifa,baadhi kuelewana bei na watuhumiwa makosa yalitokea bila kujali utu,baadhi kuficha waharifu lakini Kuna hatua walau mbalimbali za jamii kupata mwamko wa kuripoti matukio ya Ubakaji na ulawiti katika jamii ,naaamini matukio haya yatapungua kutokana na mahakama inavyoweka mkazo na kutoa adhabu kali kwa wanaofanya makosa,”amesema Chatanda.
Aidha katika kuelekea sikukuu Jeshi la polisi limeimarisha ulinzi ambapo jeshi hilo limetoa katazo kwa waendesha Disco Toto na kudai kuwa katika msimu huu wa sikukuu jeshi hilo linapiga marufuku Disco Toto.
“Tunapiga marufuku maswala ya Disco Toto ,kuna makosa mengi ambayo yamekuwa yakitokea kwenye Disco Toto ndio maana tunasema hakutakuwa na Disco Toto ,tunaomba wazazi na walezi waongeze umakini katika matembezi ya watoto wao kwa sababu dunia imechafuka, tuwe tayari kuwalinda watotO,”amesema Chatanda.



