Polisi Kisarawe wapewa elimu nishati safi

KISARAWE, Pwani: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Pwani, limeendesha mafunzo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa askari wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Kisarawe kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo na kulinda mazingira.
Mafunzo hayo pia yanalenga kufanikisha mpango wa serikali wa kuhakikisha ifikapo mwaka 2034, Watanzania wasiopungua asilimia 80 wanatumia nishati safi.
Ofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo Hadra Mtandi, amesema elimu hiyo itasaidia kuelimisha jamii kuachana na matumizi ya nishati chafu na kuchangia katika utunzaji wa mazingira.
Ofisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Esther Msaki, amesema matumizi ya nishati safi yanaboresha afya, ustawi wa jamii na kupunguza gharama za maisha.
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Tanesco Wilaya ya Kisarawe, Brighton Mmasi, amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuhakikish