Polisi Songwe kuimarisha ulinzi uchaguzi mkuu

SONGWE: ZIKIWA zimebaka siku mbili kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limesema limeweka mikakati ya ulinzi kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika maeneo yote ya mipaka ya nchi jirani za Zambia na Malawi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari akitoa taarifa kwa umma kuhusu ulinzi na usalama wakati wa kuelekea uchaguzi huo.
“Mkoa wa Songwe tunapakana na nchi mbili ambazo ni Malawi upande wa Wilaya ya Ileje na Zambia upande wa Halmashauri ya Mji Tunduma, tumekuwa na vikao vya ushirikiano na wenzetu wa nchi jirani kuhakikisha tunashirikiana linapotokea suala la uvunjifu wa amani katika maeneo ya mipaka na kukimbilia nchi hizo jirani amesema,”kamanda Senga.
Amesema wanaojipanga kufanya uhalifu na kukimbilia nchi jirani za Zambia na Malawi siku ya uchaguzi, jeshi hilo limejipanga kwa uwajibikaji wa majukumu kwa kushirikiana na kupeana taarifa na nchi hizo.
Amesema jeshi hilo limeendelea kuwa imara kiulinzi kwa kuimarisha doria katika vituo vyote vya kupigia kura, barabara kuu na maeneo yenye mikusanyiko ya watu, ikiwa ni pamoja na kufanya doria kimtandao ‘cyber patrols’.
Pia Afande Senga amewakumbusha wananchi kuepuka kushawishiwa na watu au makundi yenye nia ya kuvuruga amanii na utulivu wa mkoani wa Songwe.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com