Polisi Tabora waahidi uchaguzi wa amani

JESHI la Polisi mkoani Tabora limefanya mazoezi ya hiari katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, amesema mazoezi hayo ni maandalizi muhimu kwa jeshi hilo kuhakikisha wananchi wanatekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura wakiwa katika mazingira ya amani na utulivu.

Amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwa shwari kabla, wakati na baada ya uchaguzi, huku akiwataka wananchi, hususan vijana, kuepuka vitendo vya uchochezi na upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii.

Aidha, amewahimiza wakazi wa Tabora kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kurejea nyumbani kwa utulivu baada ya kumaliza zoezi hilo. SOMA: CP Kombo:Uchaguzi utakuwa wa amani

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button