Polisi yaomba radhi kauli ya RPC
DODOMA – Jeshi la Polisi nchini limeomba radhi kwa walioguswa na kuchukizwa na kauli ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya aliyenukuliwa na vyombo vya habari akisema “aliyedaiwa kubakwa na kulawitiwa alikuwa kama anajiuza.”
Polisi imesema kauli hiyo siyo msimamo wa Jeshi la Polisi na kwamba mwandishi aliuliza swali kuwa inadaiwa mwathirika wa tukio hilo alikuwa anajiuza, na majibu ya kamanda yalikuwa “hata kama anajiuza, hangestahili kutendewa hivyo.”
SOMA: UCHUNGUZI MSICHANA ALIYEFANYIWA UKATILI WAPAMBA MOTO
Watetezi wa haki za binadamu na utawala bora walionesha kuchukizwa na taarifa hizo na kuelezea maskitiko yao katika mitandao ya kijamii wakitaka haki kwa msichana huyo.
Msemaji wa Polisi, DCP David Misime amesema kupitia taarifa kwa umma kuwa Jeshi la Polisi litawafikisha watuhumiwa wa vitendo hivyo Mahakamani leo Agosti 19.