PPRD: Hukumu ya Kabila ni ya kisiasa

DR CONGO : CHAMA cha People’s Party for Reconstruction and Democracy (PPRD) cha Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila, kimedai kuwa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi yake ni ya kisiasa na haina haki.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Emmanuel Ramazani Shadary, amesema hatua hiyo inalenga kumtenga Kabila na siasa za taifa hilo.Mahakama ya Kijeshi ilimhukumu Kabila adhabu ya kifo baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuunga mkono waasi wa M23, waliodhibiti maeneo ya mashariki mwa Congo.

Hukumu hiyo imetolewa bila Kabila kuwepo mahakamani, hali iliyozua maswali kuhusu mchakato mzima wa kesi hiyo.Hata hivyo, baadhi ya wanasheria akiwamo Richard Bondo, walioshiriki katika kesi hiyo, wameridhishwa na uamuzi wa mahakama.

Mashirika ya haki za binadamu yameonya hukumu hiyo inaweza kuongeza mgawanyiko katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini, lakini lililokumbwa na vita na machafuko kwa zaidi ya miongo mitatu.SOMA: Kabila akabiliwa na hukumu ya kifo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button